Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, matini ya taarifa iliyotolewa na Kataib Sayyid al-Shuhadaa kuhusiana na maadhimisho ya tarehe 13 Aban, H.S, ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
“Ni mara ngapi kundi dogo limeweza kulishinda kundi kubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu! Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.”
(Suratul Baqarah, aya ya 249).
Tarehe 13 Aban ni siku ya kuporomoka nguvu na haiba bandia ya Marekani, na mwanzo wa historia ya kudhalilishwa Pentagon katika eneo hili la kijiografia. Ni tukio la kishujaa lililothibitisha kuwa utashi wa wana wa Uislamu unaweza kuzivunja sanamu za kiburi na ubeberu.
Leo hii, kufuatia kutolewa agizo thabiti la Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, linalotaka kujibiwa kwa pigo kali uchokozi wa adui mvamizi, Muqawama wa Kiislamu wa Iraq (Kataib Sayyid al-Shuhadaa), ukiwa na vidole vilivyo tayari kwenye vifyatulio vya silaha na vifua vilivyojiandaa kwa mapambano, unatoa onyo lake la wazi na lisiloweza kurejeshwa nyuma kwa viongozi wakuu wa magaidi wa Ikulu ya White House na makamanda wa Pentagon:
1. Kisasi kisichofungwa na mipaka; agizo limetolewa, hatutambui mipaka ya kijiografia
Damu takatifu za mashahidi, watoto wasio na hatia wa Ghaza na wanafunzi wasio na hatia wa Minab, kamwe haziwezi kusahaulika kwa kupita muda wala kuzuiliwa na mipaka ya kubuniwa.
Kwa kutolewa agizo thabiti la Uongozi wa Kisheria na Kidini (Wilaya), hakuna tena mpaka wala eneo la kijiografia litakaloweza kuzuia mashambulizi yetu. Kudai haki zetu hakutafanyika kupitia taasisi za bandia, bali kutatekelezwa kwa lugha ya moto na makombora ya Sajil katika medani ya mapambano. Wahalifu wa jeshi la Marekani, popote walipo katika uso wa dunia hii, wamo katika orodha ya shabaha halali na za uhakika za wapiganaji wetu, na hawatapata tena usingizi wa amani.
2. Makaburi ya eneo hili yanalisubiri jeshi vamizi la Washington
Kumalizika kwa uwepo wa kishetani wa jeshi la kikoloni katika Asia Magharibi ni uamuzi wa hakika usioweza kubadilishwa. Tunatoa onyo kwa majenerali magaidi wa Pentagon: Ima mtaondoka katika eneo hili kwa miguu yenu wenyewe, huku mkiwa katika hali ya udhalili na fedheha, au mtarejea ndani ya majeneza yaliyolazwa kwa mlalo. Kambi zote, mifumo ya rada na vituo vya uongozi na udhibiti vya wavamizi katika eneo zima vimezingirwa na makombora ya Muqawama yanayolenga kwa usahihi na ndege zisizo na rubani za kujitoa mhanga. Saa ya kuanza operesheni imekaribia, na hakuna maficho yoyote yatakayoweza kuwaokoa.
3. Jibu la kusikitisha na lenye kuangamiza kwa kosa lolote la kimkakati
Kila aina ya upumbavu, uchokozi au vitendo vya viovu vinavyofanywa na Marekani pamoja na mbwa wake mkali katika eneo hili, vitakabiliwa na jibu lililo juu ya matarajio na linalozidi makadirio yote ya Makao Makuu ya Pamoja ya Jeshi la Marekani. Kwa sasa, eneo la kijiografia la Muqawama limekuwa medani moja iliyoungana na kuhusiana kwa karibu. Moto wowote mtakaouwasha utateketeza na kuzisukuma katika maangamizi maslahi yenu yote, vikosi vyenu vya majini na njia zenu kuu za usambazaji katika eneo zima.
Onyo la mwisho kwa Shetani Mkuu:
Tarehe 13 Aban ni kioo kinachoakisi kikamilifu hatima yenu; ni siku ambayo nguvu na haiba yenu vilivunjwa jijini Tehran. Na leo hii ni siku ambayo eneo zima litageuka kuwa uwanja wa mauaji ya matarajio na tamaa zenu za kutawala.
Kwa kutii kikamilifu amri za Walii wa Mambo, hatutambui tena mpaka wowote katika kulipiza kisasi.
“Na wale waliodhulumu watakuja kujua ni marejeo gani watakayorejea.”
Muqawama wa Kiislamu wa Iraq – Kataib Sayyid al-Shuhadaa.
Tanbih: Aban ninmwezi wa nane kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Sahmsia.
Maoni yako